KAMUSI YA MISOSI

Neno kiingereza Picha Maana
Asali Honey

Asali ni chakula cha asili kinachotokana na nyuki ambacho hutumika mbadala wa sukari kwenye vinywaji na vyakula. Ni chakula muhimu sababu kimejaa virutubisho muhimu vyenye faida kwa afya ya binadamu.

Bisi Popcorn
Bizari Turmeric

Bizari, almaarufu kama kiungo cha chakula, ina ladha ya pilipili na harufu kali kiasi kwa kunusa. Ni mojawapo ya viungo muhimu kwenye chakula, hasa pilau. Bizari inatokana na mizizi, ni jamii ya tangawizi.

Bizari hutumika katika kutengeneza curry na haradali (mustard), na ndio huifanya haradali kuwa na rangi yake ya manjano.

Faida za Bizari

 • Kuzuia saratani (Cancer)
 • Kuzuia Leukemia kwa watoto
 • Inasaidia kwenye kuimarisha uzalishaji mbegu za uzazi
 • Inaimarisha kinga ya mwili
 • Inaimarisha macho na kuyafanya kuwa na afya
 • Inasaidia kuondoa mafuta yasiyo mazuri na kushusha kiwango cha kolestroli (Cholesterol)
 • Inaondoa mauvimu ya viungio vya mwili
 • Inasaidia  utendaji kazi wa ini
 • Inaimarisha chembe hai za mwili
 • Inasaidia kwenye mfumo wa usagaji chakula
 • Unasafisha mfumo wa damu mwilini
 • Inasaidia kurekebisha kiwango cha sukari mwilini.
dida
Giligilani coriander
Haradali Mustard
Hing Hing

Hing au Asafetida  ni kiungo cha chakula. Kiungo hiki ni maarufu kwa watu wa asili ya bara la Asia, hasa wahindi. Ni kiungo chenye harufu ya kipekee na kali. Hing ni kiungo kizuri kuboresha mfumo wa chakula mwilini. Kuwa makini usitumie kiasi kikubwa maana harufu yake ikizidi inaweza kukifanya chakula kisiwe na mvuto.


Picha toka kwa Manjula's kitchen

Kitunguu saumu Garlic

Kitunguu saumu ni jamii mojawapo ya kitunguu kinachotumiwa kama kiungo muhimu kwenye chakula na jamii mbalimbali duniani, mfano Afrika, Asia na Ulaya.

Faida za Kitunguu Saumu:

 • Inasaidia kuondoa matatizo ya kukatika kwa nywele kwa kuwa na kiwango kikubwa cha allicin, aina ya sulphur inayopatikana kwenye kitunguu
 • Inaondoa chunusi kwa kuwa na antioxidants
 • Inasaidia kutibu mafua, hii kama utakunywa chai yenye kitunguu saumu
 • Inaondoa muwasho wa ngozi
 • Inasaidia kuzuia mlundikano wa mafuta, hivyo kuzuia unene uliopitiliza
 • Inatibu ugonjwa wa ngozi (kama vile fungus)
 • Inasaidia kufukiza mbu
 • Inasaida kuondoa vidonda vya mdomoni vinavyotokana na homa za usiku

 

Korianda Coriander

Korianda huweza kumaanisha mbegu au majani. Korianda hutumika kama kiungo muhimu kwenye vyakula.

Faida za Korianda

 • Kiungo kinacholeta hamu ya kula na ladha nzuri kwenye chakula
 • Inasaidia kutibu matatizo ya ngozi
 • Inapunguza kiwango cha kolesteroli (Cholesterol) kwenye damu
 • Inasaidia mmengenyo wa chakula na kupunguza kuhara yanayotokana na matizo ya fungus
 • Inasaidia kuzuia na kupunguza kutapika na kusikia kichefuchefu na maumivu mbalimbali ya tumbo
 • Inasaidia kurekebisha msukumo wa damu mwilini
 • Inatibu vidonda vya mdomoni
 • Inaongeza chuma kwenye damu na kusaidia kuondokana na matatizo ya kupungukiwa chembe nyekundu hai za damu [Anaemia (Anemia)]
 • Inapunguza allergies na kuvimba kwa koo
 • Inazuia magonjwa kama Typhoid kwa kuzuia ukuaji wa vijidudu aina ya Salmonella
 • Calcium iliyopo kwenye Korianda inasaidia kuimarisha mifupa na kuisaidia kwenye kukua vizuri
 • Inasaidia kwenye mmeng'enyo wa chakula
 • Inaleta kinga dhidi ya ugonjwa wa ndui kutokana na kuwa na Vitamin C na madini ya chuma. Vilevile inasaidia katika kupunguza maumivu kwa wale wangonjwa wenye ndui.
 • Inasaidia kuondoka maumivu na kurekebisha mfumo wa hedhi kwa wakina mama kwa kurekebisha homoni (Hormone) ya endocrine.
 • Inaimarisha macho kwa uwepo wa Vitamin A, C na madini kama Phosphorous na mafuta muhimu kwa kuboresha kazi za misuli ya macho.
 • Inasaidia kurekebisha kiwango cha Insulin kwenye damu, hivyo kupunguza matatizo kwa wagonjwa wa kisukari.

Chanzo: Unaweza kusoma zaidi hapa

kotimiri Coriander
limao lemon

Tunda lenye maji machachu ambayo ni chanzo kizuri cha vitamin c. Tunda hili hutumiwa kwenye shughuli mbalimbali za mapishi na tofauti na mapishi.

 

Maji ya limao yana faida nyingi mwilini. Kati ya hizo, faida chache ni:

 • Kuongeza kinga ya mwili
 • Kusaidia kusafisha ngozi
 • Kupunguza aside mwilini
 • Kuzuia uvimbe
 • Kusaidia kulinda afya ya kinywa
 • Kusaidia kusafisha damu

 

 

Majani ya kitunguu Leeks
Mdalasini Cinnamon

Mdalasini ni maarufu kama kiungo cha chakula (au mboga) chenye harufu na ladha nzuri, lakini vilevile hutumika kama dawa kutibu magonjwa tofauti. Mdalasini ni magamba ya miti, ambayo huweza kupatikana kama unga yakisagwa na kutumika kwenye chakula. Vilevile, huweza kutumika moja kwa moja kama magamba kwenye chakula.

Faida za Mdalasini:

 • Kusaidia kutibu shinikizo la damu
 • Inasaidia kuhifadhi chakula kwa muda mrefu
 • Ina harufu nzuri kama kiungo cha chakula
 • Ina madini muhimu kwa afya – Calcium, chuma, Fiber na manganese.
 • Inasaidia kupunguza maumivu ya tumbo la hedhi kwa wanawake
 • Inasaidia kutibu ugonjwa wa baridi yabisi
Mkate Bread

Mkate ni chakula au kitafunwa maarufu kinachotengenezwa kwa kutumia unga wa ngano, hamira na maji. Mara nyingi mkate hutengenezwa kwa kuoka. Mkate ni chakuma kikuu kwa mida ya asubuhi hata hata kwenye milo tofauti Tanzania na kwenye jamii tofauti duniani kote.

PAPRIKA
Pilipili Manga Black pepper

Pilipili manga ni kiungo cha chakula chenye faida nyingi kwa afya ya binadamu. 

Hizi ni faida 10 za pilipili manga

 1. Kuboresha ufyonzwaji wa virutubisho mwilini
 2. Kuboresha mmeng’enyo wa chakula
 3. Kuleta hamu ya chakula
 4. Kusaidia mwili kupungua uzito
 5. Kuondoa gesi tumboni
 6. Kuondoa kuvimbiwa
 7. Kuondoa maumivu ya viungo
 8. Kuzuia saratani na magonjwa mengine sugu
 9. Kuondoa msongo wa mawazo
 10. Kutibu magonjwa ya fizi na meno
siagi
supu ya kidonge
Tangawizi Ginger

Tangawizi ni kiungo kinachotokana na mzizi. Mmea huu unafanana zaidi na mmea wa binzari.Tangawizi ina faida sana katika maisha ya binadamu.Tangawizi inaweza kutumika ikiwa mbichi au kavu.

 

Faida za tangawizi

 • hutumika kama kiungo kwenye chakula
 • Hutumika kama dawa
 • Husaidia kupunguza gesi tumboni
 • Hupunguza kichefuchefu
Tortilla (Chapati) Tortilla

Tortilla ni mkate ulio mfano wa chapati unaotengenezwa kutumia unga, maji na chumvi . Ni chakula maarufu sana kwa jamii ya amerika ya kusini. Hizi hutumika kupika vyakula kama tacos, burritos, or quesadillas. Wengi pia hupendelea kutengeneza sandwich, shawarma, gallete na vingine vingi.